Habari juu

RALC yakanusha habari inayo tangaza kifo cha lugha ya Kinyarwanda.

March-25
04:47 AM 2016

Watu wengi siku hizi wasema kwamba lugha ya kinyarwanda ipo njiani ikipotea. Wanawo sema hivio watowa mfano wa kuchangwa lugha vinavio dhihirika katika misemo ya watu katika maongezi ya watu.

Nsanzabaganwa Modeste Kiongozi wa RALC
RALC yakanusha habari hizo kwa kusema kwamba lugha ya Kinyarwanda ni lugha inayo simama vizuri kuliko lugha nyingi za kiafrika. "Lugha ya Kinyarwanda ni lugha inayo simama vizuri kuliko lugha nyingi barani afrika kwa maana ni lugha yenye sheria za kuilinda. Lugha huimarika inaposaidiwa na wenye nayo na ina sheria zilizo kuwa wazi, ambazo ziliandikwa, na ina msemo unao julikana" alisema Nsanzabaganwa Modeste kiongozi wwa RALC.
Watu wengi wamechukuwa hatuwa ya kufundisha lugha ya Kinyarwanda wanawo hitaji kujifunza. Haya yote yaonyesha kwamba lugha ya kinyarwanda yaendea kukuwa maana yazidi kuvuka mipaka. Zaidi ya hayo kuna vyuo vya kimataifa vinavyo funza lugha ya kinyarwanda kama Harvard University ya Umarekani, St Petersbourg ya Urusi na penginepo kama Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani na pengine.

Mtafsiri : Rene Gitangaza

Partager

Kuandika maoni yako

E-mail yanyu ntaho izagaragazwa.
Ahari aka kamenyetso * ningombwa kuhuzuza