Burudani

Tanzania : wimbo wa snura wapigwa marufuku.

May-06
11:36 AM 2016


Serikali ya Tanzania imepiga marufuku wimbo na kanda ya video ya muziki kwa jina chura wa msanii Snura Mushi kuchezwa katika vyombo mbalimbali vya habari hadi pale msanii huyo atakapoufanyia marekebisho wimbo huo.

Vilevile Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya mwanamuziki huyo hadi pale atakaposajili kazi zake katika baraza la taifa la sanaa BASATA.
Hatua hiyo inafuatia maudhui ya utengenezwaji wa video hiyo ambayo serikali inasema inakiuka maadili ya raia wa Tanzania.
Serikali imesema kuwa kazi ya mwanamuziki huyo inadhalilisha tasnia ya muziki nchini Tanzania.
Video Snura akizungumzia kupigwa marufuku video yake

Partager

Kuandika maoni yako

E-mail yanyu ntaho izagaragazwa.
Ahari aka kamenyetso * ningombwa kuhuzuza